0



LICHA ya kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi nchi na sasa mvua za
masika kuanza kunyesha maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga ikiwemo
wilaya ya Kishapu hali ya chakula ni tete kwa wananchi wilayani Kishapu.





Hali ni mbaya kattika kata za Mwamalasa,Lagana,Masanga,Shagihili na
Mondo katika wilaya hiyo yenye jumla ya kaya 42,000 na watu
wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 272,990 kwa mujibu wa sense ya mwaka
2012.




Akizungumza na Nyahore Blog, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
(MNEC)wa wilaya hiyo,Boniface Butondo jana alisema licha ya mvua
kuanza kunyesha lakini wananachi katika maeno hayo wanalazimika
kushindia uji kama mlo kamili kufuatia mazao yao kuathiriwa na jua
kali lililodumu takribani miezi mitatu sasa na kukausha mazao yao
ikiwemo mtama na mazao ya jamii ya mikunde.




Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao,pia wamemtaka Waziri wa Chakula
na Ushirika kufika na kijonea hali halisi badala ya ksubiri taarifa
kutoka katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kishapu na mkoa wa Shinyanga
ambazo wamedai zimekuwa na urasimu mkubwa katika kuupatia ufumbuzi
tatizo lililopo.




Mnec huyo alisema kuwa pia hali ya mifugo ni mbaya huku bei ya kuuzia
mifugo ikishuka kila uchao katika mnada wa Upili wa Mhunze kufuatia
mifugo kudhoofika kwa kukosa majani.

Na Anceth Nyahore, Kishapu



Butondo alisema kaya nyingi zimeishia hata ile akiba ya chakula, na
hata ile tabia na desturi ya jamii ya kisukuma ya kula milo mitatu
kuanzi uji,chakula cha mchana na kile cha usiku nap engine kuchuma
zile mboga za asili makondeni na kupika imetoweka baada ya mboga hizo
kuto ota.




Alisema hata ile njaa ya mwaka 2007 ya baadhi ya wananchi wa wilaya
hiyo katika maeneo ya vijiji vya Mwalata kata ya Masanga kushuhudiwa
na alieykuwa Waziri Mkuu wakati huo Edward Lowasa ya watu kula mashudu
ya pamba (Cotton Cake) huku mifugo ikifa kwa kukosa majani katika kata
vijiji vya Kinampanda na Magalata kata ya Mwamalasa, sasa ni zaidi
ikilinganishwa na kipindi hicho.




Wananchi hao wameiomba serikali wakati ikifuata taratibu zake za
kutafuta takwimu kupitia kitengo cha maafa ofisi ya waziri mkuu ni
busara ikawaangalia kwa jicho la huruma wanancnhi hao kwa kuanza
kuwapelekea chakula haraka kuoka uhai wao.




“Serikali ichukue hatu za haraka kuleta chakula cha dharula bila
kujali utaratibu wa kufanya tathimini kwanza kwani hali ni mbaya na
kuna hatari ya watu kupoteza maisha”alisema Butondo na kuungwa mkono
na John Ndama diwani wa kata ya Mondo.




“Hatua za haraka zichukuliwe vinginevyo raslimali watu itapotea na
waziri mwenye dhamana na serikali iliyoko madarakani haitaelekewrka
kwa wananchi wake na hata nje ya wilaya hiyo”alisema Butondo.




Kuhusu kuporomoka kwa bei ya mifugo hivi sasa ng’ombe aliyekuwa
akiuzwa shilingi milioni 1.2 anauzwa shilingi,300,000 hadi 400,000, na
aliyekuwa akiuzwa 400,000 anauzwa shilingi 100,000 na aliyekuwa
akiuzwa shilingi 200,000 anauzwa shilingi 50,000 katika mnada wa Upili
ulioko Mhunze Kishapu.




Pia mbuzi wameshuka bei kutoka shilingi 60,000 hadi 15,000 kondoo
kutoka shilingi 40,000 hadi 10,000 nao kuku kutoka shilingi 12,000
hadi 4,000.




Kuhusu juhudi za awali zilizokwishwa fanywa na viongozi wilayani humu
Butondo alisema kuwa wamefika mahali hasa wakiwemo madiwani kutoa
msadaa ya chakula kama mtama,mahindi na unga na pesa taslimu na sasa
uwezo wao umegota.




“Viongozi wamejitahidi kwa hali nanmali kukabilia hali hiyo hasa
madiwani,kutoa misaada ya chakula,mahindi,mtama,unga na pesa taslimu
lakini sasa uwezo wetu umegota”alisema Mnec huyo ambaye pia ni diwani
wa kata ya Lagana.




Aidha wamewataka viongozi wenye dhamana kutoa taarifa bila kuogopa
kuelezea hali halisi na kamwe wasiogope kuwa watavuliwa nyadhifa zao
na kundolewa madarakani kwa kuelezea majanga yaliyopo katika maeneo
yao.

Na Anceth Nyahore -Kishapu
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment

 
Top