0
Matukio ya watu kujinyonga yameendelea kujitokeza mkoani Shinyanga ambapo ,mwanamke aitwaye Sarah Lucas(25) mkazi wa kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ,amekutwa amefariki kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani kwenye banda la kuku.



Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga amesema tukio hilo limetokea Machi 29 mwaka huu majira ya saa tisa alasiri ambapo mwanamke huyo ambaye ni mke wa afisa mifugo wilayani Kishapu alikutwa amejinyonga  kwa kutumia kamba ya katani nyumbani kwake kwenye banda la kuku.

Ameongeza kuwa baada ya majirani zake kubaini kuwa mwanamke huyo kuwa amefariki ,ndipo walipotoa taarifa kwa jeshi la polisi ambalo lilifika eneo la tukio na kuukuta mwili huo ukiwa kwenye banda la kuku nyumbani kwake.

Amesema katika uchunguzi wa awali walikuta marehemu ameacha ujumbe wa maandishi unaosema kuwa "nashukuru mume wangu tumeishi wote, naomba umtunze mwanangu na kumsomesha na upo tayari kuoa mwanamke mwingine".

Post a Comment

 
Top